Hatua hiyo imechukuliwa baada ya Mamlaka hiyo kushindwa kuwalipa malimbikizo ya mishahara hiyo kwa kipindi chote.
Akizungumza na wafanyakazi wa shirika hilo, katika stesheni kuu ya Dar es Salaam, Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue, alisema ni jambo la kusikitisha kuona wafanyakazi wanafanyakazi bila kulipwa mishahara yao.
Alisema, serikali italipa mishahara hiyo, ili kutoa muda kwa mamlaka hiyo kujipanga zaidi namna bora ya kujiimarisha kiuchumi na namna ya kuboresha mazingira ya wafanyakazi wake.
Serikali ya Zambia na Tanzania kwa pamoja zimekubaliana kuipa mitaji ya uendeshaji na pia kusisitiza umuhimu wa serikali mbili kulipa mishahara ya wafanyakazi kwa kuwa Tazara haina uwezo huo kwa sasa.
Balozi Sefue alisema mbali na mishahara, lakini serikali imekuwa ikitoa fedha za kusaidia uendeshaji wa shirika hilo.
Serikali imeshalipa Shilingi bilioni 14.7 kwa ajili ya mafao ya wastaafu kati ya Mei 2005 na Desemba 2009, Shilingi bilioni 11.2 kwa ajili ya mishahara ya watumishi kati ya Juni 2013 na Mei 2015, bilioni 21.7, misamaha ya kodi na katika mwaka 2015/16 imetenga bilioni 25 kwa ajili ya kugharamia mpango wa maendeleo ya Tazara.
Alisema. Aliwasihi wafanyakazi kuwapa ushirikiano watendaji wapya wa Shirika hilo baada ya kufanyika mabadiliko ya uongozi wa juu, ili waweze kuzalisha zaidi na kulikwamua shirika hilo ambalo ni muhimili mkubwa katika kukuza uchumi na hali za maisha ya wafanyakazi hao.
Awali Katibu Mkuu wa wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaaban Mwinjaka, alimweleza Katibu Mkuu Kiongozi kwamba suala la mishahara ndio limekuwa changamoto kubwa katika mgogoro wa wafanyakazi wa Tazara, kwani wafanyakazi hao hawajalipwa tangu Januari mwaka huu.
Alisema pamoja na hesabu za Tazara kuonyesha kuwa wafanyakazi wa Tazara wanadai pesa za mishahara ya miezi ya Agosti na Oktoba, lakini kuna baadhi ambao wamelalamika kwa kutolipwa tokea mwezi Januari.
ìNawaomba kwa wale wafanyakazi wote ambao hawajalipwa watulie na kwamba mishahara hiyo itatolewa moja kwa moja kutoka wizarani na hivyo mtalipwa kilka wanapopata mishahara watumishi wa serikali.
Baadhi ya wafanyakazi walilalamikia matatizo katika uongozi wa Shirika hilo kwamba umekuwa ukiongoza kibabaishaji na kuwa na ubadhirifu kwani pamoja na kudai kuwa Tazara haina hela, lakini treni zinaonyesha kufanya kazi nyingi bila faida kuonekana.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI