.

Mabehewa
Hamsini kati ya 274 ya kusafirishia mizigo katika Reli ya Kati
yamewasili nchini kutoka India na mabehewa 22 ya abiria yana tarajiwa
kuwasili Desemba mwaka huu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya U chukuzi Dakta SHABANI MWINJAKA amesema
kuwasili kwa mabehewa hayo kutaokoa kwa kiasi kikubwa miundombinu ya
barabara ambayo huharibika muda mfupi baada ya kutengenezwa kutokana na
malori ya mizigo kwani kwa sasa mizigo yote itasafirishwa kwa njia ya
reli .
AmesemaKampuni ya Reli T anzania imetengewa zaidi ya shilingi
bilioni 45 kwa ajili ya kuboresha huduma zake ikiwa ni pamoja na kununua
vichwa na mabehewa mapya.
Amesema hadi mwaka 2015 injini 45 zitakuwa z imekamilika amba zo z
itawezesha kusafirisha tani milioni 1.5 na kuongeza kuwa u jenzi wa
reli ya kisasa kutoka Dar es salaam kwenda Kigoma, Tabora hadi Mwanza na
Uvinza Msongati hadi B urundi utafanyika.
Mkurugenzi M tendaji wa Kampuni ya Reli Tanzania M handisi KIPALLO
KISAMFU amesema injini nne zilizokuwa zikitengenezwa mkoani M orogoro
zimekamilika na nyingine 15 zinatengenezwa Afrika ya K usini amba zo z
itagharimu shilingi bilioni 70 .