Wanyama
 kama mbwa na paka wamekuwa wakithaminiwa sana na watu wa Ulaya, 
Marekani na kuna wakati unakuta mtu anambeba paka au mbwa wake kwenye 
pochi au begi kwenda naye matembezini.
Lakini hii ya mama huyu inatoka China, Xue Hsueh amewashangaza
 watu wengine kumchukulia kama mnyanyasaji na katili, yeye aliamua 
kumbeba mtoto wake wa miezi tisa katika pochi yake.
Alipiga picha huku mwanaye huyo akiwa kwenye pochi na kuisambaza kwenye mitandao, comment
 za watu wengi walimkosoa wakionyesha kuchukizwa na kitendo hicho japo 
alijitetea kwa kusema alimuweka mtoto huyo kwenye pochi kwa muda mfupi 
na kumtoa, picha hiyo alipiga kuwatania marafiki zake.

