
Jamaa mmoja Peter Angelina
ambaye ana taaluma ya udaktari lakini kutokana na kiwango chake cha
elimu kutomruhusu kufanya kazi Uingereza, aliona aendelee kutafuta
riziki kupitia biashara ya kuuza tissue pamoja na vitu vingine vidogo
vidogo katika mitaa ya Uingereza ambapo kwa hapa Tz wanafahamika kama
Machinga.
Peter aliiona briefcase
ikianguka kutoka juu ya taxi, akaifuata na kugundua kuwa ndani kulikuwa
na pesa kiasi cha Paundi 16,000 ambazo ni zaidi ya mil.40 za Tz,
akazipeleka kituo cha Polisi ili wamtafute muhusika wampatie.
“Watu
wanasema ningechukua pesa zote na kutupa ile briefcase lakini mimi siko
hivyo na hata Mungu asingependa kitendo hicho… Mimi ni mzima, sio
kichaa.. niko sawa kabisa…”—Peter.
Baada ya muhusika kufika kituoni hapo
kwa ajili ya kuchukua briefcase yake ambayo mbali na kiasi hicho cha
pesa kulikuwa na simu ya mkononi pia, mwenye briefcase hiyo alimpatia
Peter kiasi cha pesa ambacho ni sawa na laki mbili na nusu za Tz.