Ni December ambayo tunashuhudia rekodi mbalimbali zikiingia kwenye kumbukumbu za mwaka huu,tumesikia sana ya Chris Brown na Karrueche, Justin Bieber na Selena Gomez, Nick Minaj na wengineo ambao huu mwaka haukuwa na heri kwenye ulimwengu wa uhusiano wa kimapenzi.
Kumekuwa na story za mastaa wengi vijana
ambao uhusiano wao unayumba kila siku, kumbe wakati wengine wakiyumba
wapo ambao wanasherekea ndoa zao kudumu muda mrefu.
Mastaa wawili David Beckham na mke wake Victoria wameoana
tangu mwaka 1999, sherehe ya ndoa yao ni moja ya sherehe
zilizohudhuriwa na watu wachache zaidi ambapo wageni waalikwa walikuwa
29 tu.
Mpaka sasa mastaa hao wana watoto wanne,
mbali ya maisha yao kuwa ya kuhama hama lakini bado ndoa yao ni moja
kati ya ndoa za mastaa vijana ambazo zimedumu muda mrefu zaidi na bado
zinaonekana imara