Baraza
la Habari Tanzania (MCT), limetoa nafasi za mafunzo kwa wahitimu wa
vyuo vya uandishi wa habari nchini ili waweze kunolewa na kuajiriwa
katika vyombo vya habari.
Msimamizi wa Mafunzo na Taaluma ya Habari wa MCT, Pili Mtambalike, alisema hayo wakati akitunuku vyeti kwa wahitimu wa stashahada ya Uandishi wa Habari katika Mahafali ya 14, ya Chuo Cha Uandishi wa Habari (TSJ), yaliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mtambalike alisema taaluma ya uandishi wa habari ni tofauti na taaluma nyingine kutokana na kuwa katika mhimili wa tatu wa serikali, ambao kwa kutumia kalamu inaweza kutengeneza au kuharibu amani nchini na duniani.
“Baraza la habari litatoa mafunzo kwa ninyi wanafunzi mliomaliza katika kiwango cha stashahada ya uandishi ili kuwanoa muweze kukubalika katika vyombo vya habari hapa nchini na nje, mjue jinsi ya kuelimisha jamii kwa usahihi,” alisema.
Alifafanua kuwa mafunzo hayo yatafanyika kwa wale watakaoandika barua ya kuomba nafasi hizo na mafunzo hayo yatahusu uandishi wa habari za uchunguzi, ujasiri wa kufichua maovu yanayofanyika nchini na maadili ya uandishi wa habari.
Alifafanua kuwa MCT lina mpango wa kufanya mazungumzo na vyombo husika ili serikali itoe mikopo ya elimu ya juu hasa kwa vyuo vya kati, kuifanya taaluma hiyo kuimarika na kufanya kazi kwa usahihi na uelewa wa hali ya juu.
Aliwausia wahitimu hao 200, waliopata stashahada ya Uandishi wa Habari kujiendeleza hadi kiwango cha Shahada ya Uzamivu (Phd), kutokana na kazi ya kuelimisha jamii ilivyo kubwa, hali itakayowafanya kuandaa vipindi katika radio na televisheni vyenye mvuto na vilivyojaa maadili ya mtanzania ikiwa ni pamoja na mafunzo yanayoweza kumbadilisha mtu.

CHANZO:
NIPASHE JUMAPILI