
Mbunge wa Kigoma kusini, David Kafulila amesema waziri wa nishati na madini, Prof. Sospeter Muhongo alipewa muda wa zaidi ya saa moja kujitetea bungeni lakini akashindwa kuwashawishi wabunge kuwa hakuhusika na wizi wa fedha hizo, hivyo wale wanaojaribu kumkingia kifua ili rais Jakaya Kikwete asimuwajibishe wanajisumbua.
Akihutubia mkutano wa hadhara ambao umeandaliwa na vyama
vinavyounda umoja wa katiba Ukawa, na kuhuduriwa na mamia ya wananchi
katika maeneo ya uyole jijini Mbeya, mbunge wa Kigoma kaskazini, David
Kafulila amesema kuwa maazimio ya bunge ya kutaka watuhumiwa wa sakata
la Escrow wawajibishwe yapo palepale na kuwa wale wanaojaribu kumtetea
waziri wa nishati na madini Prof. Sospeter Muhongo wanahangaika bure kwa
vile Prof. Muhongo mwenyewe alishindwa kujitetea bungeni licha ya
kupewa muda wa kutosha wa kujitetea.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo
(Chadema) mkoa wa Mbeya, Joseph Mwachembe maarufu kwa jina la china
amesema kuwa amebaini kuwa wakurugenzi wote wa halmashauri mkoa wa Mbeya
wamepewa maelekezo ya siri ya kuandaa mahali pa kujiandikishia kupiga
kura, hivyo nakuwataka wananchi kuwa makini na kujitokeza kwa wingi
punde zoezi la kujiandikisha litakapoanza.
Mbunge mstaafu wa jimbo la Mbeya mjini kupitia chama cha NCCR
mageuzi, Policia Mwaiseje amesema kuwa wananchi hawana sababu ya kusoma
katiba inayopendekezwa kwa kuwa imeandikwa na mafisadi wa Escrow na
badala yake wakaikatae kwa kuipigia kura ya hapana.