
Makamu wa Raisi wa Chama cha Soka
dunia Fifa Ali Bin Al Hussein atachuana na bosi wake Sepp Blatter katika
kuwania kiti cha urasi.
Ali mwenye miaka 39 atasimama kuwania
uraisi kwenye uchaguzi utakaofanyika Mei 29 ambapo Blatter atakua
akiwania kuongoza chama hicho kwa muhula wanne.“Ni wakati wa kubadili mwelekeo wa kiutawala mbali na matatizo ya kimichezo vichwa vya habari viwe kuhusu soka sio Fifa" alieleza Ali.
Jerome Champagne, aliejiunga na Fifa mwaka 1999, akiwa ni balozi nae amedhibitisha kuwania nafasi hiyo ya juu ya uongozi.
Wagombea wanaotaka kuwania nafasi za uongozi wanatatakiwa kutangaza nia kabla ya Januari 29.