MATUKIO MAKUBWA KUTOKA KENYA.

By | 11:10
                    Nairobi-City
Walimu saba raia wa Kenya wamejeruhiwa baada ya kulipukiwa na bomu lililokuwa limetegwa kando ya barabara Somalia, mtu mmoja alifariki kutokana na mlipuko huo uliokuwa umelenga basi la shule.
Watu watatu wamefariki na majeruhi wametajwa kuongezeka kutoka na kuanguka kwa jengo la ghorofa saba huko Nairobi, Mkurugenzi wa CID Ndegwa Muhoro ameagiza wahusika wote kujisalimisha kituo cha Polisi.
Rais Uhuru Kenyatta ameitembelea familia ya Raila Odinga kuwapa pole ya kufiwa na mtoto wa kwanza wa Odinga, Fidel Odinga ambaye alifariki usiku wa kuamkia jana Jumapili katika mazingira ya kutatanisha nyumbani kwao.
Newer Post Older Post Home