
Vijana watatu kutoka nzega wametembea kwa miguu kwa siku 37 hadi jijini dar es saalam kwa lengo la kutaka kwenda kumuona Rais Jakaya Kikwete kufikisha malamiko yao ikiwemo kukithiri kwa vitendo vya rushwa na ubadilifu wa rasilimali za umma lakini safari ya vijana hao ikaishia mikononi mwa polisi baada ya kukadi agizo halali la mkuu wa wilaya ya kinondoni Mh. Jordan Rugimbana la kuwataka wafuate taratibu za kumuona kiongozi huyo wa nchi.
Vijana hao ambao walivalia magunia na kusema kuwa wamevaa hivyo
ikiwa ni ishara ya kuonyesha uchungu wa namna ambavyo rasilimali za
taifa zisivyowanufaisha wazawa.
Baadhi ya wananchi walioshuhudia matembezi hayo wamewataja vijana
hao kama ni wazalendo ambao ujumbe wao unawagusa mamilioni ya
watanzania ambo hawana ujasiri na uwezo wa kufanya kitendo cha kijasiri
kama hicho.
Baada ya vijana hao kufika kwa mkuu wa wilaya walifanya mazungumzo
naye ambapo mkuu huyo aliwataka wafuate taratibu za kumuona rais na
kusisitiza kuwa matembezi hayo yalipaswa kuishia hapo.
Kufuatia maagizo hayo vijana hao hawakukubaliana na agizo hilo na
kusema wao bado nia yao ya kwenda ikulu ipo pale pale na ndipo
walipioanza safari nyingine kuelekea huko na kabla ya hapo walitoa
matamko yao mbele ya ofisi ya mkuu wa wilaya kabla ya kukamtwa na
kupelekwa kituo cha polisi magomeni.