
Michezo ya mtoano kufanyika March 12
Matokeo
ya upangwaji wa droo ya timu 16 ya ligi ya Europa zitafanyika leo
nchini Uswisi kuanzia saa tisa kwa saa za Afrika Mashariki.
Droo
hiyo itasimamiwa na Katibu Mkuu wa UEFA, Gianni Infantino, na Mkurugenzi
wa Mashindano wa UEFA, Giorgio Marchetti, pamoja na Jerzy Dudek, Kipa
wa zamani wa timu ya taifa ya Poland, ambae ndiye Balozi wa fainali ya
Mwaka huu ya Europa Ligi itakayochezwa huko Poland, Mei 27.Droo hii itahusisha timu 16 zilizofuzu toka kwenye timu 32 ambapo jana usiku zilikamilisha michezo yao ya marudiano.
Michezo ya mtoano itapigwa kuanzia Machi 12 na Marudiano Machi 19 na Washindi kutinga hatua ya Robo fainali.