
Mbunge wa Arumeru Magharibi, Joshua Nassari.
Mwanasiasa huyo aliyekuwa mmoja wa wana CCM waliowania uteuzi wa
kuwania ubunge Jimbo la Longido mwaka 2010 na kuangushwa na Mbunge wa
sasa Lekelu Laizer, alijiunga Chadema jana, akitaja sababu kuu tatu
zilizomfanya kuchukua uamuzi huo.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Namanga,
mpakani mwa Kenya na Tanzania, muda mfupi baada ya kukabidhiwa kadi ya
Chadema na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, Ikayo alisema
amevutiwa na mikakati ya chama hicho ya kutetea haki za wanyonge.
“Nina sababu kuu tatu za kuhamia Chadema. Mosi ni kwa sababu chama
hiki kimejipambanua kuwa watetezi wa wanyonge, pili kuna uhuru na
demokrasia ya kila mtu mwenye uwezo kugombea bila kuwekewa mizengwe na
tatu kinapiga vita rushwa, ufisadi na matumizi mabaya ya mali na fedha
za umma,” alisema Ikayo.
Wazee watatu kutoka jamii ya wafugaji wa Kimasai anakotoka Ikayo,
Lekishoo Loodo, Moi Lesingo na Laidinga Nangoro, walimkabidhi rungu na
usinga mwanachama huyo mpya wa Chadema, ikiwa ni ishara ya kukabidhiwa
majukumu ya Kiuongozi.
Akihutubia mkutano huo, Ikayo aliitaka jamii ya wafugaji kuamka na
kuacha kuwa mtaji wa ushindi wa CCM nyakati za uchaguzi, kwa kile
alichoeleza chama hicho kimewatelekeza kwa kuruhusu maeneo ya malisho
kuvamiwa, huku wafugaji wakilazimika kuhangaika na mifugo yao kutafuta
malisho.
Kwa upande wake, Lema aliwataka watu wote wenye umri na sifa za
kujiandikisha kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye Daftari la
Wapiga Kura, ili kupata fursa ya kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu
baadaye mwaka huu.
Kwa upande wake, Mbunge wa Arumeru Magharibi, Jashua Nassari
aliwaomba wachungaji, maaskofu na masheikh kote nchini, kuacha kupokea
fedha haramu zinazotokana na wizi wa fedha na mali za umma zinazotolewa
makanisani na misikitini na wasaka madaraka.
CHANZO:
NIPASHE