
Hali ya maisha imekuwa ngumu kwa kijana huyu Abdallah Omar umri wake ni miaka 17, ana kipaji cha uandishi wa script za movie, akabahatika kukutana na Geah Habib wa ‘Leo Tena’ @CloudsFM ambaye alimkutanisha pia kijana huyu na Zamaradi Mketema ambaye anafanya show inayohusu movie, “Take One” kwenye Clouds TV.
Kijana huyo amesimulia kwamba aliwahi
kwenda Hospitali ya Amana na kuonana na daktari, baada ya kumueleza nia
yake ya kuuza figo daktari alimweleza matatizo ambayo yangeweza kumpata
kijana huyo akitoa figo yake kwa umri wake.
Timu ya ‘Leo Tena’
imemuahidi kumsaidia kijana huyo kumkutanisha na watu walio kwenye
industry ya movie ili atumie talent yake ya uandishi wa script kupata
kipato badala ya kuuza figo.