Ubongo wa mwanadamu huhitaji mazingira mazuri ili uweze kufanya kazi vizuri
Utafiti unasema kuwa Madarasa yaliyobuniwa vizuri huinua kiwango cha elimu kwa wanafunzi wa shule za Msingi.
Watafiti
kutoka Chuo cha Salford wamesema muundo wa darasa namna lilivyojengwa
na mapambo yana mchango katika kufanya vizuri kwa Wanafunzi kwenye
kusoma, kuandika na hesabu.Darasa lenye kuruhusu Mwanga wa asili, hali ya hewa na hewa safi ni muhimu katika mafanikio ya mwanafunzi kielimu.
Watafiti hao walifanya utafiti wao wakihusisha madarasa 153 katika shule 27 kwa kipindi cha miaka mitatu.
Matokeo Makubwa
Mwandishi wa Ripoti hiyo, Profesa Peter Barret, amesema kuwa Wanadamu ni Wanyama,na Ubongo hufanya kazi vizuri kwenye mazingira mazuri na ya asili, lakini pia Mvuto wa mazingira yenyewe machoni.
Profesa Barret amesema timu yake ilishangazwa kuona kuwa Ubunifu kwenye darasa umechangia kwa kiasi kikubwa matokeo mazuri kuliko vitu vingine kama vile ukubwa wa shule,vifaa vya kitaaluma na maeneo ya kuchezea.