Mbwa
mmoja wa Polisi huko New Jersey Marekani wenye umri wa miaka
nane aliyefanya kazi kwa miaka minne amelazimika kustaafu kutokana na
afya
yake kuwa mbaya.
Mbwa huyo wa Polisi ambaye anaitwa Judge
amepewa heshima na kuagwa kishujaa,
kaandaliwa na gwaride pamoja na
kupigiwa saluti na Polisi tukio ambalo lilishuhudiwa
pia na watu wa haki za
wanyama.
Judge
alikuwa anastaafu kama mbwa wa Polisi kwenye kituo kimoja West
Deptford, New Jersey ambapo alitakiwa kustaafu tangu mwaka 2013,
kutokana na maradhi ya meno na pia afya yake kuwa sio nzuri.

Watu wa haki za wanyama walishauri mbwa
huyo ‘astaafishwe’ na pia apelekwe
kupatiwa matibabu katika Hospitali ya
wanyama ya Swedesboro.


Huu ni msafara wa gari zilizombeba mbwa huyo.


Tukio hilo sio geni sana kwa wenzetu,
kuliwahi kuwa na story ya ishu ya
mbwa mmoja wa Polisi ambaye alizikwa
kwa heshima kama ambavyo huwa
mazishi ya askari yanafanyika.
