
Utamaduni wa watu duniani unatofautiana, moja ya story ambazo sikuwahi kufahamu ni juu ya huu utamaduni wa jamii ya watu wa Dani iliyoko Magharibi mwa Papua, New Guinea ambapo utamaduni wao unahusisha inapotoke msiba wa ndugu yoyote basi ndugu wa marehemu wanaomboleza kwa kujikata vidole.
Utaratibu
huo huwa unakuwa na ibada ya utangulizi ili kufukuza mapepo ya marehemu
halafu linafuatia zoezi la kukata vidole, kwa utamaduni huo maumivu ya
mwili huonyesha huzuni ya kufiwa pamoja na kuonyesha upendo kwa
marehemu.
Hapa vidole vinakatwa kwa shoka, vipande
vilivyokatwa vinachomwa moto halafu majivu yanahifadhiwa au kuzikwa
pamoja na mwili wa marehemu.
Jitihada zimeanza kufanywa ili kuzuia utamaduni huo ambao madhara yake yameanza kuonekana kwa sasa
