Kijiji cha Mbashi kilichopo wilayani Monduli, kimepata maji safi ya bomba kwa matumizi ya wakazi wake pamoja na mifugo yao.
Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa, alisema mwishoni mwa wiki akiwa katika ziara ya kikazi kutembelea maeneo yaliyogundulika kuwa na magadi soda, kwamba kukamilika kwa mradi huo ni hitimisho la utekelezaji wa ahadi yake.
Alisema anaandaa utaratibu wa kwenda kuzindua maji hayo hivi karibuni akiwa pamoja na wageni wake na akaomba kijiji nacho kiwaalike wageni kutoka vijiji jirani.
“Tangu Tanzania ipate uhuru, Mbashi haijawahi kupata maji salama...Nashukuru katika kipindi changu cha ubunge nimefanikiwa kufikisha maji Mbashi…nimefurahi sana na hata shule na kituo cha afya sasa vimefanya vizuri,” alisema.
Alisema hapo zamani Mbashi lilikuwa eneo la kupeleka ng’ombe walioibwa sehemu nyingine lakini sasa hali hiyo imekwisha.
Akiwa katika Kijiji cha Engaruka Juu, Lowassa, alisema ametekeleza ahadi zake za kuwaletea maji safi ya bomba, umeme ambao unakaribia kuwaka.
Hata hivyo, wananchi walimweleza kuhusu mawasiliano ambapo alisema, tayari Halmashauri ya Wilaya ya Monduli imekwishatiliana mkataba na kampuni moja ya simu za mikononi na kabla hajamaliza kipindi chake cha ubunge wakazi wa kijiji hicho wataweza kupata mawasiliano kama wenzao.
Akizungumzia kuhusu magadi soda, Lowassa alisema, “sehemu kubwa ya magadi soda ipo katika Kijiji cha Mbashi na siyo Engaruka na hiyo ni kwa mujibu wa Shirika la Mendeleo la Taifa (NDC) .”
Kufuatia hali hiyo alisema hakuna mtu mwenye haki ya Mbashi kuliko wananchi wa kijiji hicho, hivyo pale walipo ni kwao mpaka kufa.
Hata hivyo alisema kiasi cha fedha ambacho Tanzania itakuwa inaingiza kwa mwaka kutokana na kuuza magadi soda ni sh. milioni 480 kwa mwaka, fedha ambazo alisema ni nyingi.
Alisema kwa mfano, mtu mmoja alimfuata akiwa Dar es Salaam akidai eti ana ardhi yake kule Engaruka lakini baada ya kumcheki akagundua kwamba ni muongo. Alitoa angalizo kwamba wakiuza mashamba yao watabaki kuwa watu wa kuzurura ovyo mijini.
Alisema maeneo ambayo tayari yamekwishapimwa kwa ajili ya uchimbaji wa magadi soda, utaratibu umeandaliwa wa kutoa fidia kwa kila mkazi ambaye atatakiwa kupisha eneo lake.

CHANZO:
NIPASHE JUMAPILI