
Ligi
kuu ya Tanzania Bara itaendelea mwazoni mwa juma hili (Jumatatu) na
swali pekee kwa wapenda kabumbu ni kwamba je Yanga, iliyonzishwa mwaka
1935 itatawazwa kuwa mabingwa wapya?. Jibu litakuwa ndio endapo vijana
hao wa jangwani watawafunga Polisi Morogoro katika mechi itakayochezwa
uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Yanga, wawakilishi pekee katika
ukanda wa Afrika ya Mashariki katika michuano ya vilabu barani Afrika
ambao watacheza na Etoile du Sahel ya Tunisia mjini Tunis katika mechi
ya marudiano ya raundi ya 16 ya michuano hiyo wikiendi hii baada ya sare
ya 1-1 jijini Dar es Salaam, wana pointi 52, ambazo kimahesabu
hazitaweza kufikiwa na timu yoyote wakati ligi hiyo ikielekea ukingoni
mwezi ujao.Baada ya mechi ya leo, Yanga, ikiwa chini ya kocha Mdachi, ambaye hivi karibuni ameiweka timu hiyo katika wimbi kubwa la ushindi, itabakiwa na mechi mbili tu mkononi na haina cha kupoteza hata ikifungwa kwani tayari imemuweka mwali kibindoni
Hata kama mabingwa watetezi, Azam FC, itafanikiwa kumaliza mechi zake zote za ligi, haitaweza, hata kwa miujiza kuifikia Yanga, ambayo haijashinda taji la ligi kuu kwa zaidi ya miaka 2 iliyopita

Kwa sasa vita ya nafasi ya pili ili kupata tiketi ya michuano ya kombe la Wawakilishi barani Afrika (Confederation Cup) ipo kati ya mabingwa watetezi, Azam na Simba yenye pointi 41 ikiwa na mechi mbili mkononi.
Simba, iliyonzishwa zaidi ya miaka 70 iliyopita, ikiwa chini ya kocha Mserbia, Goran Kopunovic ina Sali na kuomba du azote ili Azam iweze kuteleza katika mechi zake zilizobaki ili irudi katika chati ya michuano ya kimataifa, baada ya kuwa nje mwa miaka kadhaa.
Endapo Yanga watafanikiwa kuchukua ubingwa , wataiwakilisha Tanzania katika michuano ijayo ya kombe la Washindi barani Afrika
BBC SWAHILI.