MATUMAINI YA LIVERPOOL YADIDIMIA.

By | 11:43
             
Liverpool
Matumaini ya Liverpool kuorodheshwa katika nafasi nne bora yalididimia baada ya kutoka sare ya bila kwa bila dhidi ya West Brom Albion katika uwanja wa Hawthorns.
Wakati huohuo klabu ya Tottenham ilitoka nyuma mara mbili ili kusawazisha na kuinyima Southampton pointi tatu katika shindano la kuwania nafasi ya kucheza katika taji la Yuropa msimu ujao.

Graziano Pelle aliwapatia Southampton bao la kwanza baada ya masihara ya safu ya nyuma ya Tottenham lakini Lamela alisawazisha na kufanya mambo kuwa 1-1.
Hathivyo Pelle aliiweka mbele kwa mara ya pili Southampton lakini uongozi huo haukuchukua dakika tano kabla ya Necer Chadli kusawazisha kufuatia pasi murua ya Eric Diers.
Newer Post Older Post Home