MCHEKI HAPA NG'OMBE ALIYEWAGEUZA KONDOO CHAKULA CHAKE.

By | 07:19
                          cow
Mwaka 2007 huko India kulitokea habari yakushanga kidogo baada ya ndama kunaswa akimla kuku na kuleta taharuki kubwa kwa wakazi na kuleta sintofahamu
Hii tena imetokea huko Kenya na kukaa kwenye headlines baada ya mkulima mmoja kusema kuwa mmoja wa ng’ombe wake amesusia lishe yake ya kawaida na kuanza kuwala kondoo wake.
Mkulima huyo Charles Mamboleo, ambaye anamiliki shamba Kusini Magharibi mwa Nakuru aligundua kuwa ng’ombe wake amemla kondo siku moja asubuhi wakati akimpa chakula lakini jitihada zake za kumpa ng’ombe huyo chakula na maji hazikufua dafu, na siku iliyofuata ng’ombe huyo alimla kondoo mwingine.
Kulingana na afisa mmoja wa kilimo alisema huenda tabia ya ng’ombe huyo imetokana na ukosefu wa madini yanayopatikana kwa mimea mibichi.
Newer Post Older Post Home