Messi,Suarez na Naymar wakishangilia bao
Miamba
ya soka ya Hispania Barcelona, wamefanikiwa kutinga fainali baada ya
kuibwaga Bayern Munich kwa jumla ya mabao 5-3 yaliyopatikana katika
mikondo yote miwili waliyokutana kwenye hatua ya nusu fainali.
Katika mchezo wa usiku wa kuamkia leo ambao ulipigwa ndani ya dimba la Allinza Arena, Bayern walipaswa kushinda goli nne bila ili kupata tiketi ya kusonga mbele. Lakini mpaka kipyenga cha mwisho kinapulizwa the Bavarian 3, Barcelona ikipata mabao 2.
Na baadae leo usiku kutakuwa na mchezo kati ya Real Madrid dhidi ya Juventus kwenye dimba la Benabeu.