
Watu wanne wamejeruhiwa katika ajari ya basi
iliyotokea katika eneo la Tanesco barabara ya Kenyatta Jijini Mwanza.
Ajali hiyo ilitokea hii leo
majira ya saa kumi na moja za alfajiri kwa imehusisha basi la Bunda express
lenye namba za usajili T 318 CXZ, lililokuwa likitokea Kituo Cha Mabasi Buzuruga
kuelekea Kituo cha Mabasi Nyegezi ambapo.
Chanzo cha ajali hiyo ni
baada ya dereva kushindwa kukwepa gari la kushindilia barabara lililokuwa
limepaki katika Barabara Kenyata eneo la
eneo la Tanesco ambapo kuna matengenezo ya barabara.
Dakitari wa zamu wa hospitali ya Rufaa ya Bugando ambapo majeruhi hao wamepelekwa Edwini Mbwambo aliwataja majeruhi hao kuwa ni Alfan Yusufu (50),Christian Iyakugilwa (65), Richard Malema (30),Valentine Kalamagangara (30) pamoja na Donata miaka (26).
Baadhi ya Mashuhuda wa ajali
hiyo walieleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi ambapo dereva wa basi
hilo alishindwa kulimudu na hatimae kugonga gari la kushindilia barabara na
hatimae kupinduka.
Hadi tunakwenda mitamboni, Kamanda
wa Polisi Mkoani Mwanza alikuwa hajapatikana ili kuthibitisha kutokea kwa ajali
hiyo.
BINAGA MEDIA BLOG.