Maandalizi ya kombe la Dunia
Shirika
la kupigania haki za binadamu la Amnesty International ,linasema Qatar
inalazimika kuboresha hali ya wafanyakazi wahamiaji wakati huu nchi hiyo
inapoendelea na maandalizi ya kombe la dunia la mwaka 2022.
Wafanyikazi wa kigeni ndio wanaotumika kujenga viwanja Qatar
Amnesty wanasema Qatar imepiga
hatua kidogo sana kutekeleza ahadi nyingi walizozitoa mwaka jana, kwani
wafanyakazi bado wanahitaji ruhusa kutoka kwa waajiri wao ,kubadili
ajira au kuondoka nchini humo,mabadiliko ya malipo kwa wafanyakazi
yanafanyika taratibu mno wakati ni jambo la muhimu mno.