Kura ya maoni kuhusu ndoa za wapenzi wa jinsia moja Ireland
Shughuli
ya upigaji kura inaendelea huko Ireland katika kura ya maoni ya
kubadilisha katiba ili kuruhusu ndoa za mapenzi ya jinsia moja.
Iwapo mabadiliko hayo yataidhinishwa,Ireland itakuwa nchi ya kwanza kuhalalisha ndoa za wapenzi wa jinsia moja kwa wingi wa kura.
Matokeo ya kura hiyo yanatarajiwa jumamosi mchana.