
Serikali
ya Korea Kusini inasema inaamini kuwa Korea Kaskazini inaweza kumiliki
nyambizi kadha za kufanya mashambulizi kutoka baharini ndani ya miaka
mitano inayokuja.
Hii ni baada ya Korea Kaskazini kuchapisha picha
zilizomuonyesha kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong Un akitazama majaribio
ya kuizindua nyambizi hiyo.Korea Kusini imezikagua picha hizo za uzinduzi kwenye vyombo vya habari vya Korea Kaskazini na kusema kuwa ni za kweli.
Korea Kusini ilisema kuwa uzinduzi huo ni suala linalochukuliwa kwa umakini na tahadhari kubwa sana.
Sasa Korea Kusini na Marekani zinafikiria kuweka ngao ya mitambo ya kuzuia makombora kutoka Kaskazini hatua itakayogharimu mabilioni ya pesa.
Wadadisi wanasema kuwa Korea Kaskazini inaonekana kufanya mambo kwa kasi zaidi kuliko ilivyokisiwa kuunda zana zilizo na uwezo wa kushambulia kwa haraka.
BBC SWAHILI.