Usiku wa jana Uongozi wa klabu ya Liverpool ulitoa
zawadi kwa wachezaji wa timu hiyo ambao waliisaidia kwa kiasi kikubwa
katika msimu mzima wa ligi kuu, sherehe zilifanyika katika ukumbi wa Echo Arena .
Nahodha anayeondoka Steven Gerrard ameshinda
tuzo ya mafanikio ya muda mrefu ndani ya timu hiyo na anatarajia
kuichezea timu hiyo kwa mara ya mwisho dhidi ya Stoke Jumapili kabla ya
kuhamia LA Galaxy ya Marekani.
Baada ya kupokea tuzo hiyo nahodha huyo
aliwashukuru makocha wake pamoja na wachezaji wenzake kwa ushirikiano
waliouonyesha kwa kipindi chote alichoichezea klabu hiyo.
Kwa upande wa Manchester United pia walitoa tuzo kwa wachezaji wao ambapo kipa David de Gea anayetajwa kutaka kuhamia Real Madrid alishinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Manchester United na mchezaji mwenzake wa kimataifa wa Hispania, Juan Mata ameshinda tuzo ya bao Bora la Msimu alilofunga katika mechi dhidi ya Liverpool.


