Uchaguzi mkuu wa kumpata Rais mpya wa Shirikisho la soka duniani FIFA unatarajia kufanyika May 29 huku wagombea wakiwa katika maandalizi ya mwisho kabla ya uchaguzi huo kufanyika.
Wakati zikiwa zimebaki siku chache kabla ya kufanyika habari mpya ni kuhusu mgombea wa kiti hicho Michael Van Praag kujiondoa kwenye kinyang’anyiro.
Kujiondoa kwaRais huyo wa shirikisho la
soka la Uholanzi sasa kumewaacha wagombea wawili pekee wanaowania kiti
hicho pamoja na rais wa FIFA Sepp Blatter.
Wagombea wengine wanaowania nafasi hiyo ni mchezaji wa zamani kiungo kutoka Ureno Luis Figo pamoja na Rais aliyeko madarakani kwa sasa Sepp Blatter ambaye anapewa nafasi kubwa ya kushinda ikiwa ni muhula wake wa tano.