Mwana
wa kifalme wa Uingereza Prince William amesema kuwa, ameanza kupata
hemwa hemwa juu ya mchezo wa fainali ya FA itakayopigwa hapo kesho kati ya
Arsenal dhidi ya Aston Villa.
Prince Willium ambaye ni shabiki mkubwa wa Aston Villa, anasema atakuwepo katika dimba la Wembley
kutazama mpambano huo huo pamoja na kukabidhi kombe kwa timu
itakayoibuka kidedea. " nina wasiwasi na hofu" alisema Prince.Mwana huyo wa kifalme ambaye ndiye rais wa chama cha soka cha Englan FA, pia ameiambia BBC juu ya matumaini yake ya kuona wanawe wakifuata nyayo zake za kuwa mashabiki wa Aston Villa. Ushabiki wa Prince William kwa timu hiyo, umeanza tokea akiwa shuleni kwakuwa aliamini kuishabikia Aston Villa kungemfanya awe na hisia nzuri, japo ametanabaisha kuwa marafiki zake walikuwa ni Mashabiki wa Manchester Utd na Chelsea