Watoto elfu 250 huenda wakafa kwa njaa Sudan
Mshirikishi
mkuu wa shirika la Umoja wa mataifa nchini Sudan Kusini, Toby Lanzer,
amesema kuwa takriban watoto laki mbili na nusu wamo katika hatari ya
kufa katika kipindi cha miezi kadhaa ijayo iwapo mashirika ya utoaji
misaada, hayatafikisha misaada kwa watu walio na mahitaji.
Vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan Kusini imesambaratisha uchumi wa taifa hilo.
Bwana Lanzer amewasihi viongozi wa pande hasimu kusameheana ilikukomesha maafa.