
Diaby anaungana katika orodha hiyo na beki wa Aston Villa Ron Vlaar ambaye klabu hiyo bado inajaribu kuafikiana naye mkataba mpya na Wes Brown ambaye kandarasi yake imekamilika katika klabu ya Sunderland.
Chelsea nayo inamtoa Didier Drogba ikiwa ni mchezaji wa pekee anayeondoka klabu hiyo kwa uhamisho wa bure huku klabu ya Hull City pia ikiwatoa wachezaji wake 13 akiwemo Mayonor Figueroa,Paul McShane na Yannick Sagbo.