ICRC:RAIA WANAHITAJI CHAKULA SUDAN KUSINI.

By | 13:38

Sudan kusini
Kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu ICRC inasema kuwa maelfu ya watu nchini Sudan Kusini wanahitaji pakubwa chakula, maji na huduma za matibabu.
Wakiwa wamelazimishwa kukimbia makwao kufuatia kuwepo kwa mapigano, hawana njia nyingine ya kuweza kujikimu. Mazao ambayo walitarajia kuvunaa yameozea shambani.
Makundi yaliyo na silaha yanaiba mifugo na chakula, yakiwa pia yanawavamia raia.
Makundi ya kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundi yanatoa huduma kwa wale waliojeruhiwa huku pia wakijaribu kuwapelekea chakula karibu watu 6000.
Hata hivyo ICRC inasema kuwa ikiwa mapigano hayatasitishwa mara moja na misaada mingi kuwasili eneo hilo, basi maelfu ya watu wako kwenye hatari ya kukumbwa na njaa wiki chache zinazokuja.
ICRC inatoa ombi la dola milioni 23 kusaidia oparesheni yake nchini Sudan Kusini, ikiwa ndio oparesheni ya pili kwa ukubwa inayondeshwa na shirika hilo baada ya ile la Syria.
Newer Post Older Post Home