
Zaidi ya shule 700 Korea Kusini
zimefungwa kuhofia kuenea kwa ugonjwa uliozuka kwa ugonjwa unaoshambulia
mfumo wa upumuaji uliozuka kutoka Mashariki ya kati wa MERS
Watu
watatu hadi sasa wanadaiwa kufa kutokana na ugonjwa huo ambapo pia watu
wengine 35 wamebainika kuwa na maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo.
MERS ni mara ya kwanza kugunduliwa nje ya Saudi Arabia, kwani miaka
mitatu iliyopita mgonjwa wa kwanza aligunduliwa huko Mashariki ya Kati.
Rais wa Korea Kusini Park Geun-Hye amehimiza jitihada zaidi kukabiliana
na ueneaji wa virusi vya ugonjwa huo. Raia wa Korea kwa sasa wamekumbwa
na wasiwasi kutokana na ugonjwa huo wa SARS ulioua mamia ya watu huko
Kaskazini Mashariki mwa Asia zaidi ya muongo mmoja uliopita.