SWANSEA YAMSAJILI ANDRE AYEW.

By | 03:41
Andre Ayew
Mshambuliaji wa Ghana Andre Ayew amejiunga na klabu ya Swansea kwa uhamisho wa bure na kuandikisha mkataba wa miaka minne na klabu hiyo.
Ayew mwenye umri wa miaka 25,amekuwa katika klabu ya Marseille tangu mwaka 2006 lakini mkataba wake na klabu hiyo ya Ligue 1 ulikamilika mwezi uliopita.
Mchezaji huyo aliyetajwa kuwa mchezaji bora na BBC mwaka huu alifunga mabao 52 katika mechi 181 katika kilabu hiyo na amelichezea taifa lake mara 62.
''Nilihisi kwamba huu ndio wakati mwafaka kwangu'',alisema Ayew. Nilihisi hamu ya kucheza katika ligi ya Uingereza na kutaka kukuwa kama mchezaji na kwamba Swansea ndio suluhu kwangu kwa njia yoyote''.
"Uaminifu na hamu ya klabu hiyo ulinifanya kujihisi kwamba ni kweli wananitaka.Wameonyesha hilo kwa kila njia''.
Newer Post Older Post Home