MAHAKAMA YA UHALIFU KUANZISHWA SUDANI KUSINI.

By | 00:11


Image captionPande hasimu nchini Sudani kusini zinashutumiwa kutekeleza vitendo vya mauaji ya raia wasio na hatia
Umoja wa Afrika umesema mahakama maalumu itaundwa kwa ajili ya kuwashitaki washukiwa wa makosa ya uhalifu wa kivita nchini Sudani kusini ambapo imekumbwa na mzozo mkubwa tangu mwaka 2013.
Hatua hii inalenga kuunga mkono hatua ya Afrika kushughulikia migogoro yao wenyewe hivyo pia Sudani kusini kupata fursa ya kufanya hivyo pia.
Uchunguzi umebaini kuwa Serikali na vikosi vya Waasi vimetekeleza mauaji.
Ingawa makubaliano ya amani yalitiwa saini mwezi uliopita, bado mgogoro umeendelea.
Uundwaji wa mahakama ni sehemu ya makubaliano ya Rais Salva Kiir na Kiongozi wa waasi, Riek Machar yaliyotiwa saini baada ya kuwepo shinikizo kutoka kwa viongozi wa kikanda.
Sudani kusini haiitambui mahakama ya kimataifa ya icc, Umja wa Afrika pia umeikosoa mahakama hiyo kwa kufanya kazi zake kwa upendeleo, madai ambayo ICC imekana.
bbc swahili.
Newer Post Older Post Home