MAJESHI YA NATO YAWASILI KUNDUZ.

By | 02:36


Image copyrightReuters
Image captionKikosi maalum cha shirika la kujihami la muungano wa mataifa ya Magharibi NATO, kinasemekana kufika mji wa Kunduz nchini Afghanistan.
Kikosi maalum cha shirika la kujihami la muungano wa mataifa ya Magharibi NATO, kinasemekana kufika mji wa Kunduz nchini Afghanistan.
Nia hasa ni kujaribu kuutwaa tena mji huo, ambao kwa sasa uko chini ya udhibiti wa kundi la wapiganaji wa Taliban.
Waasi hao waliudhibiti mji huo siku ya Jumatatu, baada ya kuanzisha makabiliano makali kutoka pande zote.
Image copyrightReuters
Image captionUjasusi unasema kuwa kinara mkuu wa Taliban mjini Kunduz Mawlavi Salam, ameuwawa karibu na uwanja wa ndege
Idara ya ujasusi wa Afghanistan, inasema kwamba kinara mkuu wa Taliban mjini Kunduz Mawlavi Salam, ameuwawa karibu na uwanja wa ndege.
Msemaji wa jeshi la Marekani Peter Cook, amesema kwamba majeshi ya NATO yamewasili mjini huo ili kutoa ushauri wa kijeshi kwa walinda usalama wa taifa hilo.
Amesema pia kuwa, jeshi la Marekani lilitekeleza shambulio la angani viungani mwa mji huo ili kuzima hatari ya mkusanyiko wa muungano wa wapiganaji.
Image copyrightReuters
Image captionMarekani ilitekeleza mashambulio ya angani viungani mwa mji huo ili kuzima Taliban
Rais Ashraf Ghani amewaambia wanahabari mjini Kabul kuwa wanamgambo wanawatumia raia kama ngao.
Shirika la kimataifa la madakari wasio na mipaka Medicins san Frontieres, mapema walisema kuwa hospitali mjini Kunduz imejaa majeruhi wa vita.
Newer Post Older Post Home