DJIBOUTI YAFUNGWA 6-0 MECHI YA KUFUZU KOMBE LA DUNIA

By | 10:29


Kombe la Dunia
Image copyrightEPA
Image captionMshindi kati ya Niger na Somalia atakutana na Cameroon Novemba
Niger imelaza Somalia 2-0 kwenye mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi.
Moussa Maazou alifunga mabao mawili kipindi cha pili na kuwezesha taifa hilo la Afrika Magharibi kutia kibindoni alama zote tatu.
Mechi hiyo ilichezewa mji mkuu wa Ethiopian Addis Ababa.
Maazou, ambaye huchezea soka ya kulipwa Uchina, alifunga dakika ya 58 na kisha akafunga mkwaju wa penalti dakika nne baadaye.
Mataifa hayo mawili yatakutana kwa mechi ya marudiano Jumanne ijayo.
Mshindi atasonga na kukutana na Cameroon kwenye raundi inayofuata ya kufuzu mwezi Novemba.
Kwingineko, Djibouti walikuwa hawana lao baada ya kupokezwa kichapo cha 6-0 na Swaziland, mechi iliyochezewa uwanja wa El Hadj Hassan Gouled mjini Djibouti.
Mabao ya Swaziland yalifungwa na Mthunzi Mkhontfo (45'+1), Sabelo Ndzinisa (62'), Muzi Dlamini (74'), Sandile Hlatjwako (77'), Tony Tsabedze (83') na Mxolisi Lukhele (85').
Newer Post Older Post Home