Michuano ya timu za taifa za Ukanda wa Afrika Mashariki Kati (CECAFA) ambayo wengi tumeizoea kwa jina la michuano ya Challenge inatarajia kuanza kufanyika Novemba 21 hadi December 6 2015 Ethiopia. Michuano hiyo ambayo mwaka jana haikufanyika kwa kawaida ushirikisha jumla ya nchi 12.
Michuano ya Challenge inatajwa kuwa michuano mikongwe zaidi barani Afrika na mara ya mwisho ilifanyika Kenya na nchi mwenyeji kutwaa ubingwa huo, michuano hiiTanzania ugawanyika kwani Zanzibar hupeleka timu yao ya Zanzibar Heroes lakiniTanzania bara hupeleka kikosi chao cha Kilimanjaro Stars.
Kupitia Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF limethibitisha Oktoba 2 kuwaKilimanjaro Stars itashiriki michuano hiyo itakayoanza Novemba 21 hadi December 6Ethiopia. Nchi wanachama wa ukanda wa Afrika Mashariki na kati ambao wanatarajia kushiriki ni Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Sudan, Sudan Kusini, Tanzania bara,Zanzibar, Ethiopia, Djbout, Somalia na Eritrea.