
Mfungwa aliyetoroka gerezani nchini Australia wiki kadha zilizopita amekamatawa akiwa amejificha kabatini.
Mwanamume huyo wa umri wa miaka 58 alitoroka jela ya St Helier mjini Muswellbrook katika jimbo la New South Wales Julai 24.
Alikamatwa na maafisa wa polisi akiwa amejificha kwenye kabati jikoni katika nyumba moja eneo la Alfords Point, kilomita 264 kutoka gereza hilo.
Polisi jimbo la New South Wales wanasema atashtakiwa kutoroka gerezaji.