MMEA UNAOKULA WADUDU.

By | 17:24


Image captionMmea unaokula wadudu
Mmea mmoja unaokula wadudu unatumia nguvu za matone ya mvua ili kuwakamata wadudu hao,wanasayansi wamebaini.
Wanasayansi hao kutoka chuo kikuu cha Bristol wamebaini kwamba matone hayo ya mvua husababisha mtikisiko katika majani ya mti huo ambayo yana umbo la mtungi.
Hatua hiyo huwapeleka wadudu katika mfuniko wa mtungi huo wenye mtego, ambapo wadudu hao huzamishwa na kuliwa.
Matokeo ya utafiti huo yaliochapishwa katika jarida la PNAS yanatokana na kamera zenye kasi na zisizo na mtikisiko mkubwa.
Image captionKifaa kinachofanana na mmea huo.
Kwa matumizi ya vifaa hivyo ,daktari Ulrike Bauer pamoja na wenzake walirekodi kasi na mtikisiko unayoendelea katika majani ya mti huo baada ya kuangukiwa na matoni hayo ya maji.
Hatua hiyo ni ya kipekee miongoni mwa mimiea , Daktari Bauer anasema.
''Kasi yake ambayo husaidia kuwakamata wadudu pamoja na vile mmea huo unavyotumia nguvu za nje ni suala la kushangaza''.
Newer Post Older Post Home