NI HARAMU KUTOA PEREMENDE BADALA YA CHENJI KENYA.

By | 05:21


Image captionNotisi iliotolewa na benki kuu Kenya.
Benki kuu ya Kenya imetoa taarifa katika magazeti ya leo nchini humo ikiyataka maduka kusita kutoa vitu mbadala vya masalio ya sarafu ya taifa hilo.
Baadhi ya maduka yamekuwa yakitoa mda wa maongezi ya simu,viberiti na hata peremende badala ya kutoa masalio yanayohitajika kulingana na mwandishi wa BBC Joseph Odhiambo.
Image captionSarafu
Lakini benki kuu imesema kuwa kuna aina ya sarafu za kutosha na kuziagiza benki zote nchini kuhakikisha kuwa sarafu hizo zinasambazwa.
Newer Post Older Post Home