
Watoto
wa rais wa Marekani Barrack Obama,Sasha na Malia wameshtumiwa kwa
kukosa heshima na afisa mmoja wa chama cha Republican baada ya
kuhudhuria sherehe za kutoa Shukran.
Elizabeth Lauten ,ambaye ni
mkurugenzi wa mawasiliano wa mbunge Stephen Fincher alitoa matamshi yake
katika mtandao wa facebook ambayo baadaye yalifutwa.Baada ya kukosolewa Bi Lauten aliomba msamaha kwa kutoa matamshi hayo ya kukera.
Alikua akikosoa sketi fupi zilizovaliwa na wasichana hao wa Obama.
Bi Lauteni pia aliwashtumu wasichana hao kwa kuonyesha uchovu wakati waliposimama na baba yao katika sherehe hiyo ya ikulu ya Whitehouse.
''Mama yenu na baba yenu hawa heshimu nyadhifa zao kama inavyohitajika na taifa kwa jumla.
kwa hivyo naona kwamba munakosa ile hadhi ya kuwa kioo cha jamii.Maandishi hayo yaliendelea na kuwashauri wasichana hao kuonyesha kwamba wanaishi katika ikulu ya Whitehouse.
Vaeni mavazi ya kuonyesha munahitaji kuheshimiwa sio kama muko katika baa.