
Wakili wa Darren Wilson ambaye ni afisa wa polisi aliyempiga risasi na
kumuua kijana mweusi Michael Brown kwenye eneo la st Louis nchini
Marekani mwezi Agosti anasema kuwa polisi huyo amejiuzulu.
Mapema wiki hii bwana Wilson aliondolewa mashtaka hatua iliyozua ghadhabu miongoni mwa waamerika weusi.Afisa huyo amekuwa likizoni tangu mauji hayo yafanyike, mauaji ambayo yalisababisha majuma kadha ya maandamano.
Gazeti hilo lilichapisha kile lilichodai kuwa barua yake ya kujiuzulu ambayo ilisoma:''nimearifiwa kwamba iwapo nitaendelea kuwa mfanyikazi wa idara ya Polisi basi hatua hiyo itawachochea maafisa wa polisi na raia wa eneo la Furguson kuishi kwa hofu,hali ambayo siwezi kuikubali hata kidogo.''