Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza bungeni Dodoma jana.
Dar/Dodoma. Moto wa kashfa ya
ufisadi katika akaunti ya Tegeta Escrow unaoendelea kuwaka
bungeni, sasa unaonekana kugeuka gharika inayoweza kuwakumba vigogo wengi zaidi na kuiweka
Serikali ya Rais Jakaya Kikwete katika hali ngumu.

Kashfa hiyo ya uchotaji wa Sh306 bilioni za
akaunti ya Escrow, inahofiwa kuwakumba vigogo
zaidi ya 50 ndani ya Serikali wakiwamo mawaziri, makatibu wakuu, wabunge, majaji na
wakuu wa taasisi za Serikali waliohusika.

Habari zilizopatikana zinaeleza kuwa kutokana na
kuwapo kwa idadi kubwa ya mawaziri na
watendaji wa Serikali na mahakama, inatishia anguko la Serikali.

“Kuna waziri (anamtaja) ameniambia ameangalia ile
orodha ya watu wanaodaiwa kuchukua
fedha hizo ni zaidi ya 52. Hofu yangu hili jambo likiingia bungeni na kujadiliwa huenda
likasababisha kuvunjwa kwa Baraza la Mawaziri kwa mara nyingine,” alisema mbunge
mmoja kutoka Kanda ya Mashariki.

Wabunge wajipanga
Mbunge mwingine kutoka Zanzibar (CCM), alisema
kuwa anasubiri kwa hamu
kuchangia katika mjadala huo ili waondoke wale wote ambao wamekwapua fedha hizo.

Juzi, Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliitisha kikao
cha mawaziri ambacho kilihudhuriwa na
baadhi ya mawaziri na walifikia uamuzi kuwa suala hilo litajadiliwa ndani ya chama
kabla ya kuingia ndani ya Bunge.

“Kinachosubiriwa ni ripoti ya Kamati ya Hesabu za
Serikali (PAC) halafu tutakutana
wabunge wa CCM kabla ya kwenda bungeni,” alisema mmoja wa wajumbe wa kikao hicho.

Pamoja na hali hiyo, wabunge katika makundi
makundi kwa wiki nzima wamesikika wakijadili
jambo hilo huku wakilihusisha na mbio za urais mwakani.

Mbunge mmoja (jina tunalo) alisema kuhusishwa kwa
Waziri Mkuu Mizengo Pinda katika
sakata hilo kunatokana na mtuhumiwa mmoja ambaye ni kiongozi katika Wizara ya
Nishati na Madini, kuwa mmoja wa meneja wake wa kampeni.

“Hakuna mahali ambapo Pinda ameguswa moja kwa moja
katika ripoti ya
CAG (Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali) wala Takukuru
(Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa), bali wanasema ni kwa sababu ya kampeni
za urais na mhusika mmoja katika sakata hilo anatajwa kuwa kama Pinda akipata urais,
yeye ndiye atakayekuwa Katibu Mkuu Kiongozi,” alisema mbunge huyo kutoka upinzani.

Jana Mbunge wa Kilwa Kaskazini (CCM), Murtaza
Mangungu akizungumza na gazeti hili,
alisema sakata hilo linatakiwa liishe kwa kuwa linaumiza uchumi wa nchi kwa kuwa
mtambo wa IPTL ni matatizo.

“Hili jambo kwa namna yoyote lazima liishe na kwamba mwisho wake ni bora tutaifishe ule
mtambo na ufie mbali,” alisema Mangungu.

Alisema linatakiwa liishe kwa kuwa limekuwa ni
jambo la kushutumiana kila upande kitu
ambacho si kizuri, na kwamba Bunge linapaswa kusimama kuonyesha makali yake.

“Ni mzigo kwa wananchi hivyo lifike mwisho. Ni heri shari yenye heri kuliko heri yenye shari
,” alisema Mangungu.
,” alisema Mangungu.
Mbunge wa Ole (CUF), Rajabu Mohammed Mbarouk
alisema sakata hilo limetokea juu na
sasa limefika chini na kukwamisha mambo mengine yasifanyike.

“Bunge haliwezi kuisha kwa kuwa linagusa masilahi
ya watu wengi, pia linagusa masilahi ya
chama. Hili hata lijadiliwe bungeni haliwezi kuisha hivyo,” alisema Mbarouk.

Alisema ni jambo la ajabu kama alivyosema Zitto
kwamba halikufaa kufanyika kwenye
nchi ambayo ina dola, bali lingefanyika kwenye nchi ambazo hazina mhimili wa dola kama Somalia.

“Haya mambo yanaweza kumwangusha Waziri Mkuu na wengine, hivyo ni jambo zito,”
alisema Mbarouk.
alisema Mbarouk.
Mbunge wa Kasulu Mjini (NCCR-Mageuzi), Moses
Machali akiwasilisha maoni ya kambi
ya upinzani kuridhia Itifaki ya Uzuiaji wa Vitendo Haramu dhidi ya Miundombinu jana,
alisema viongozi kama wabunge na mawaziri wametajwa kupiga dili katika akaunti ya
Tegeta Escrow kwa kuwa viongozi wa Serikali hawaonyeshi dhamira njema katika
kuheshimu misingi ya utawala bora na ndiyo maana wezi na mafisadi wanaotakatisha
fedha kiharamu wameendelea kuachwa.

Alisema katika uchotwaji wa fedha hizo, Serikali
imedhihirisha wazi kwamba ufisadi ni
sehemu ya maisha ya baadhi ya mawaziri na watendaji wa Serikali.

“Ni aibu na majanga kwa Waziri Mkuu na mawaziri
wengine kusema kwamba suala la
Escrow haliwezi kuzungumzwa bungeni kwa sababu eti liko mahakamani, jambo
linaloashiria Waziri Mkuu anakusudia kuwalinda wale wanaotajwa kuchota fedha hizo,
” Machali alisema na kuongeza:

“Mbaya zaidi ni pale inapoonekana wazi mhimili wa
Bunge unaingiliwa na mhimili mwingine
unaotajwa kuliandikia Bunge barua likitaka kutojadiliwa sakata la Escrow jambo ambalo
ni dharau kwa Bunge.”

Kwa upande wake, Zitto ambaye kamati yake inapitia
ripoti hiyo hakutaka kuzungumzia chochote
kuhusu sakata hilo lakini juzi aliwataka wabunge wajiandae kupambana na taarifa atakazoziwasilisha
mezani mara tu ripoti hiyo itakapokabidhiwa bungeni kwa
ajili ya majadiliano

Escrow yavuka mipaka ya nchi
Sakata la utoroshwaji wa fedha katika akaunti ya
Escrow ambalo linawaandama baadhi ya watendaji
wakuu wa Serikali limejitokeza kwa sehemu kubwa katika baadhi ya magazeti ya nchi za Magharibi
yaliyohoji jinsi Serikali inavyoingiwa na kigugumizi
cha kulipatia ufumbuzi sakata hilo.

Magazeti hayo likiwamo DailyMail la Uingereza
ambalo lililowahi kufichua kuwapo kwa vitendo
vya ufisadi katika uwindaji wa wanyamapori kulikolisababishia taifa hasara kubwa, lilisema kuwa
Tanzania inaendelea kuandamwa na
jinamizi la ufujaji wa mali ya umma.

DailyMail limesema wabunge wameibana Serikali
wakitaka kujadiliwa kwa ripoti ya Escrow
ili kuliokoa taifa ambalo tayari limeanza kuonja machungu ya kusitishiwa misaada kutoka kwa
wafadhili wa kigeni.

Katika ripoti yake hiyo ambayo imelinukuu Shirika
la Habari la Reuters, DailyMail ilisema
rushwa ni ugonjwa unaoendelea kuiandama Tanzania na kwamba vitendo hivyo sasa vimevuka
mipaka na kuwakwaza wawekezaji wa kigeni.

Limesema kuwa Tanzania ambayo hivi karibuni
ilitangaza kugundua hifadhi kubwa ya gesi
iko katika njiapanda na bado haieleweki hatima yake hasa baada ya Serikali kuonyesha kuwa
haiko tayari kuruhusu ripoti hiyo ijadiliwe hadharani.
.iko katika njiapanda na bado haieleweki hatima yake hasa baada ya Serikali kuonyesha kuwa