
Mawaziri nchini Zambia wamemtaka Rais anayeshikilia madaraka kwa sasa ya nchi hiyo Guy Scott kuachia ngazi kwa madai hawana imani nae kwa kiongozi mweupe kushikilia madaraka ikiwa haijawahi kutokea zaidi ya miaka 20 iliyopita.
Scott alipewa madaraka ya kuiongoza nchi hiyo baada ya kufariki kwa rais wa nchi hiyo Michael Satta aliyefariki mwezi Oktoba mwaka huu mjini Lusaka.
Mawaziri 14 kati ya 17 walihudhuria mkutano ulioitishwa na kupiga kura ya kutaka Rais huyo aachie madaraka kwa kukosa imani naye kutokana na asili yake.

Awali Chama tawala cha nchi hiyo Patriotic Front nachokilionekana kutokua na imani nayo hivyo Scott kuwa katika wakati mgumu wa kuingoza nchi hiyo.
“Tunamtaka Rais anayeshikilia kiti hicho kwa sasa Scot kujiuzulu nafasi hiyo mara moja”alisema Waziri wa mambo ya nje Harry Kalaba.
Scott amekua katika wakati mgumu kutokana na kutokua raia wa nchi hiyo lakini hata hivyo imebakia mwezi mmoja kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa nchi hiyo.