
Kwa nchi nyingi za Afrika hasa Tanzania
zinapiga marufuku kubwa ya uonyeshwaji wa movie za ngono kutokana na
kwamba hazina maadili mazuri kwenye jamii, ukienda nchi kama China wao
wameenda mbali zaidi, sheria kali zimewekwa ili kuzuia kabisa mtu yeyote
kucheza filamu hizo, ama kuuza.
Nchi za Ulaya na Marekani zimekuwa
zikishutumiwa kuruhusu biashara zote, kutengeneza na kuuza movie hizo,
lakini hii kutoka Los Angeles, Marekani imeweka sheria inayowalazimu
waigizaji wa filamu hizo za ngono kuvaa mipira maalum ya kuwakinga na
maambukizi ya magonjwa, Condom.
Sheria hii ambayo ilianza kama muswada
mwaka 2012 inawalazimu waandaaji wa filamu hizi pia kulipia ada maalum
ili kupewa kibali cha kufanyia kazi hiyo.
Wadau wa industry ya filamu hizo wamedai
kuwa wanafahamu fika hatari zilizoko kwenye maambukizi na wanachukua
hatua za kupunguza maambukizi haya kwa kuwakinga na kuwapima watu wote
wanaoshiriki uigizaji wa filamu hizi kabla ya kuingia nao mikataba
ambapo utaratibu huu mpya unawapa hofu waandaaji hao kwamba huenda soko
la biashara yao likayumba.