
Spika
wa Bunge la Afrika Mashariki Margaret Nantongo Zziwa aondolewa
madarakani na wabunge wa Afrika Mashariki baada ya kupigwa kura ya
kutokuwa na imani naye.
Jumla ya wabunge 39 walishiriki katika kikaao cha bunge hilo
kilichofanyika asubuhi ya leo chini ya mwenyekiti wa bunge la Afrika
mashariki idadi ya kura zilizounga mkono kuondolewa kwa spika huyo ni
36, mbili zilisema hapana na moja kuharibika.