
Mbunge wa arumeru mashariki Joshua
Nasari aliyekamatwa jana jioni leo amefikishwa katika mahakama wilaya ya
arumeru na kusomewa shitaka la kuharibu mali kwa kuchana bendera ya
chama cha mapinduzi CCM katika kijiji cha EMBASENI na kuachiwa kwa
dhamana.
Mbunge huyo alifikishwa mahakamani hapo majira ya saa tano asubuhi
na kusomewa shitaka la kuharibu mali kwa kuchana bendera ya CCM na
hakimu wa mahakama ya wilaya ya meru David Mwita kuwa mnamo tarehe 16
mwezi Desemba mtuhumiwa alitenda kosa hilo katika kijiji cha EMBESERI
ambapo mtuhumiwa alikana kosa na kuachiwa kwa dhamana ya shilingi
milioni moja na nusu pamoja na wadhamini watatu na kesi yake itatajwa
tena tarehe 24 mwezi huu.
Baada ya kutoka mahakamani akiwa nje ya mahakama mbunge huyo amesema
anashangaa kupewa kesi hiyo kwa kosa ambalo hajawahi kutenda lakini hiyo
inatokana na wivu wa kupata vitongoji vingi katika uchaguzi wa serikali
za mitaa kwa mara ya kwanza na atorudi nyuma kwa vitisho hivyo.
Naye mbunge wa arusha mjini Godbles Lema amesema fitina hizo
zitafika mwisho kwani mashariti aliyowekewa mbunge huyo yanaonesha kuwa
walitaka kumkomoa lakini chadema ipo imara na kamwe Haitarudi nyuma.