
Wengi wetu ni wapenzi wa vitafunwa, maandazi, keki, mikate ni baadhi tu ya vile ambavyo tumezoea kuvitumia majumbani kwetu kwa ajili ya kifungua kinywa.
Kuna wakati mwingine hatujui vitafunwa hivi vinaandaliwa katika mazingira gani.
Jina maarufu la mama huyo anaitwa ‘mama T‘ alikiri kufanya kosa hilo baada ya kupigwa na watu wenye hasira.
Jamaa ambaye ni mmoja ya watu
walishuhudia tukio hilo amesema alikuwa anaoga, ghafla akatokea panya
aliyetaka kumuuma mguu, akampiga na mti panya akafa, muda mfupi baadaye
panya aliongezeka ukubwa na baadaye kuwa mtu halafu akakimbia akiwa
amevaa kandambili moja na moja akaiacha.
Alipotoka ili akasimulie wenzake alikuta kundi la watu waliomzunguka mama huyo akiwa amevaa kandambili moja mguuni.
Baada ya ushahidi huo walimpiga akakubali kufanya vitendo vya kishirikina na pia kutengeneza mikate hiyo ambayo inaitwa ‘moi-moin’ akitumia mkojo.