
Baada ya kumshuhudia nahodha wake Steven Gerrard akiitoa salamu kwamba anaitumikia klabu hiyo katika msimu huu kama utakuwa msimu wake wa mwisho baada ya miaka 26 katika klabu hiyo wekundu wa Anfield wataongozwa na mchezaji mwingine .
Henderson alijiunga na Liverpool misimu mitatu iliyopita akitokea Sunderland na baada ya kuanza kwa kasi ya chini amekuja kuwa mchezaji muhimu kwenye klabu hiyo kiasi cha kuaminiwa na kuwa nahodha mpya.

Kocha wa Liverpool, Brendan Rogers ameamua kuwa Jordan Henderson atarithi nafasi ya Steven Gerrard kama nahodha wa klabu hiyo.
Pamoja na kuwepo kwa taarifa kuhusu Henderson
kukabidhiwa mikoba kama nahodha mpya, bado haijafahamika nani atakuwa
nahodha msaidizi kwenye klabu hiyo na inaaminika kuwa huenda kiungo
mshambuliaji Raheem Sterling akateuliwa kuwa nahodha msaidizi.