Mama mmoja mjamzito alikwenda
Hospitali ya Mkoa Morogoro siku ya jana, alipofika hospitali hapo
hakupata huduma nzuri kutoka kwa nesi aliyekuwa zamu, baada ya uchungu
kumshika alihangaika bila msaada wowote na mwisho wake akajifungua
chini.
Wakati huo ilikuwa usiku, umeme ulikuwa umekatika na wakalazimika kutumia tochi ya kwenye simu wakati akijifungua.
Ndugu walimchukua mtoto huyo akiwa
amewekwa ndani ya ndoo, walipofika nyumbani waligundua kwamba mtoto
alikuwa mzima bado lakini waliporudi tena Hospitali jitihada za kumtibu
hazikusaidia kwani alifariki wakati wakianza jitihada za kumshughulikia.
Mganga Mkuu Hospitali ya Mkoa Morogoro amesema kuwa hakuwepo kwa kuwa yupo likizo.
